Askari magereza wa nchini Uganda aliyetambulika kwa jina la Lawrence Ampe amefukuzwa kazi baada ya kuikosoa serikali kupitia mtandao wa TikTok, huku mamlaka zikisema alichokifanya ni utovu mkubwa wa nidhamu na kuongeza kuwa Kanuni za kazi haziruhusu mtumishi wa umma kushiriki siasa.
Lawrence Ampe amekuwa akichunguzwa kutokana na machapisho yake kwenye mitandao ya kijamii yaliyowatuhumu maafisa wakuu wa serikali kwa rushwa, ukiukwaji wa haki za binadamu na kuwatendea vibaya maafisa wa magereza wa ngazi za chini.
Upinzani umelaani hatua hiyo, ukiieleza kuwa ni ushahidi wa ukandamizaji wa kimfumo ndani ya sekta ya usalama.
Chanzo; Eatv