Nchi ya Marekani imetajwa kushika nafasi ya 128 kati ya mataifa 163 yenye amani duniani kwa 2025, (nchi yenye amani kidogo) nyuma ya nchi kama Afrika Kusini ambayo inashika nafasi ya 124, Kenya ikishika nafasi ya 127 na Uganda 114 hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Uchumi na Amani (IEP).
Ripoti hii huangazia zaidi suala la usalama wa jamii, migogoro inayoendelea ndani ya nchi husika na ulinzi na masuala ya kijeshi. Amani imetajwa kupungua duniani kwa 0.36% mwaka 2025 huku nchi 87 zikikosa amani na nchi 17 zikitajwa kuwa na vifo zaidi ya 1,000 vinavyohusiana na migogoro.
Chanzo: Crown Media