Rais Donald Trump amesema Marekani imefanya shambulio kali na hatari dhidi ya kundi la Islamic State (IS) kaskazini magharibi mwa Nigeria.
Kiongozi huyo wa Marekani amesema IS ni magaidi wakubwa na kulishutumu kundi hilo kwa kuwalenga na kuwaua kikatili, Wakristo wasio na hatia.
Trump amesema jeshi la Marekani limefanya mashambulizi hayo, huku Kamandi ya Marekani ya Afrika (Africom) ikiripoti kwamba shambulio la Alhamisi lilifanywa kwa ushirikiano na Nigeria katika jimbo la Sokoto.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, Yusuf Maitama Tuggar ameiambia BBC ni operesheni ya pamoja inayolenga magaidi, na haina uhusiano wowote na dini fulani.
Chanzo; Nipashe