Watu 63 wamepoteza maisha baada ya mabasi mawili ya abiria kugongana uso kwa uso kwenye mji mdogo wa Kiryandongo, magharibi mwa Uganda.
Polisi ya nchi hiyo imesema watu wengine kadhaa wamejeruhiwa katika ajali hiyo ambayo ndio mbaya zaidi kuwahi kutokea kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki mnamo miaka ya hivi karibuni.
Kulingana na taarifa ya polisi mabasi mawili ya abiria yaliyokuwa yakitokea upande tofauti yaligongana yalipojaribu kuyapita magari mengine katika barabara kuu inayoelekea mji wa Gulu uliopo kaskazini mwa Uganda.
Chanzo: Dw