Makamu wa Rais wa zamani Kamala Harris ameweka wazi nia yake ya kugombea tena nafasi ya Urais wa Marekani katika uchaguzi wa mwaka 2028 kupitia Chama chake cha Democratic wakati akifanya mahojiano na Kituo cha BBC jana Jumamosi.
Katika mahojiano hayo Bi Kamala amesema kuna uwezekano wa siku moja yeye kuwa Rais wa Taifa hilo kubwa duniani na kuandika histori ya kuwa mwanamke wa kwanza tena mweusi kuwa rais.
Kamala Harris alishindwa na Donald Trump katika uchaguzi wa mwaka 2024 baada ya aliyekuwa Rais kwa wakati ule Joe Biden kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho siku 107 tu kabla ya Siku ya Uchaguzi.
Chanzo: Crown Media