Mwandishi wa habari wa Sudan, Muammar Ibrahim, amekamatwa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika mji wa El-Fasher, Darfur Kaskazini. Ibrahim alikuwa akiripoti kuhusu hali ya vita na mateso ya raia katika eneo hilo.
Taarifa zinasema alikuwa miongoni mwa waandishi wachache waliobaki kuripoti kwa vyombo vya habari vya kimataifa tangu vita kuanza. Hali ya usalama mjini humo imeendelea kuwa mbaya kutokana na mapigano makali kati ya RSF na jeshi la Sudan.
Mashirika ya kutetea haki za waandishi wa habari yamelaani kukamatwa kwake. Yameitaka RSF kumwachilia huru mara moja na kusisitiza kuwa uandishi wa habari si uhalifu.
Chanzo: Global Publishers