Rais Donald Trump wa Marekani amesema meli za mafuta ambazo aliamuru zikamatwe nje kidogo mwa pwani ya Venezuela zitabakia kuwa mali ya Marekani.
Akijibu maswali ya waandishi habari mjini Washington, Trump amesema serikali yake itachukua umiliki wa meli hizo na kuashiria kwamba zinaweza kutumika kuhifadhi mafuta.
Tangu Disemba 10, Marekani imezikamata meli mbili za mafuta inazozituhumu kukwepa vikwazo vya Washington kwa biashara ya mafuta ya Venezuela.
Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amezitaja hatua hizo za Marekani kuwa "vitendo vya kijambazi na uharamia wa kimataifa".
Chanzo; Dw