Iran imeendelea usiku kucha kuvurumisha makombora ya masafa na droni kuilenga Israel na washirika wa Marekani kwenye eneo la ghuba, ikiwemo shambulizi kubwa lililoulenga ubalozi wa Marekani nchini Saudi Arabia.
Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia imesema ndege mbili zisizo na rubani zimeushambulia ubalozi huo wa Marekani mjini Riyadh na kusababisha moto mkubwa ambao hata hivyo tayari umedhitiwa.
Rais Donald Trump ameapa kuiwajibisha Iran kwa uamuzi wake wa kuushambulia ubalozi wa nchi yake na kwa mauaji ya wanajeshi 6 wa Marekani tangu kuanza kwa vita Jumamosi iliyopita.
Mashambulizi ya kujibu mapigo ya Iran yamezifikia pia nchi za Bahrain na Kuwait huku makombora yake yaliyoelekezwa Israel yameanguka kwenye makaazi ya watu na kusababisha uharibifu.
Chanzo; Dw