Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Marekani Yatoa Sababu ya Kupigana na Iran

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth, amesema lengo la mashambulizi ya nchi hiyo dhidi ya Iran ni kuharibu miundombinu ya kiusalama na kuzuia taifa hilo kuzalisha silaha za nyuklia.

Akizungumza usiku wa jana Machi 2, 2026 wakati akitoa taarifa kuhusu operesheni iliyopewa jina la ‘Epic Theory’, Hegseth amesema lengo la misheni hiyo ni kushambulia na kudhoofisha uwezo wa kijeshi wa Iran kwa kulenga maeneo muhimu ya kimkakati.

“Dhamira ya misheni ‘Epic Theory’ ni mahsusi kabisa; kuharibu miundombinu ya Iran kuzalisha silaha, kuharibu jeshi lao la wanamaji na miundombinu mingine ya kiusalama. Iran haitawahi kuwa na silaha za nyuklia,” amesema Hegseth.

Kauli hiyo imekuja huku kukiwa na mapigano yanayoendelea kati ya Marekani kwa kushirikiana na Israel dhidi ya Iran, ambapo pande zote zimekuwa zikitoa matamko makali kuhusu hatua za kijeshi na usalama wa kikanda.

Aidha, ameonya baadhi ya vyombo vya habari vinavyoripoti kuwa vita hivyo vinaweza kuchukua muda mrefu, akivitaka kuacha kusambaza taarifa hizo kwa kauli ya mkato, 'stop it'.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: