Mtu wa pekee nje ya familia ya Kim kuhudumu kama rais asiye na mamlaka nchini Korea Kaskazini, Kim Yong Nam, amefariki dunia.
Haya ni kulingana na shirika la habari la kitaifa la Korea Kaskazini, KCNA, lililotoa tangazo hilo leo.
Kim Yong Nam ambaye alihudumu katika nafasi hiyo chini ya viongozi wote watatu wa nchi hiyo, amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 97.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametoa heshima zake kwa kiongozi huyo mapema leo.
Nam alihudumu katika wadhfa huo kuanzia mwaka 1998 na akastaafu mwaka 2019 na ndiye aliyekuwa kama sura ya diplomasia ya Korea Kaskazini.
Chanzo; Dw