Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Marco Rubio, ameionya Israel dhidi ya mipango ya kulitwaa kwa nguvu eneo la Ukingo wa Magharibi linalozingatiwa kimataifa kuwa ardhi halali ya Wapalestina.
Matamshi ya Rubio yanafuatia hatua ya Bunge la Israel, Knesset, kuidhinisha katika hatua ya awali miswada miwili ya sheria itakayotoa nguvu kwa serikali ya nchi hiyo kulipoka eneo la Ukingo wa Magharibi na kuliweka chini ya himaya yake.
Rubio amesema hali hiyo inatishia kuteteresha utulivu kwenye kanda hiyo ikiwa ni pamoja na makubaliano ya amani yaliyofikiwa hivi karibuni ya kumaliza vita vya Ukanda wa Gaza.
Chanzo: Dw