Rais wa Marekani Donald Trump amesema Israel na Hamas wametia saini awamu ya kwanza ya mpango wa amani ya Gaza.
Kundi la Hamas linatarajiwa kuwaachilia huru mateka 'hivi karibuni' likisema mateka wa Israel walio hai watabadilishwa kwa karibu wafungwa 2,000 wa kipalestina.
Trump alisema Jumatano kwamba anaamini mateka wote walioshikiliwa huko Gaza, ikiwa ni pamoja na miili ya marehemu, "watarudi" Jumatatu.
Israel nayo itawaondoa wanajeshi wake kwa njia iliyokubaliwa. Msemaji wa serikali ya Israel ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba Israel inatarajia mateka wake wataanza kuachiwa Jumamosi.
Msemaji huyo hakusema iwapo serikali inatarajia mateka wote 48 waliosalia, wanaoishi na waliokufa, wataachiliwa wote mara moja.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu atakutana na baraza lake la mawaziri leo Alhamisi ili kuidhinisha mpango wa kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa huko Gaza.
Chanzo: Dw