Serikali ya Nigeria imetangaza mabadiliko makubwa kwenye vyeo vya juu vya kijeshi, ikibadilisha Mkuu wa Utawala wa Ulinzi pamoja na wakuu wa jeshi la nchi kavu, jeshi la majini na jeshi la anga.
Hatua hiyo inachukuliwa chini ya wiki moja baada ya vyombo vya habari nchini humo kuripoti kwamba kulikuwa na jaribio la mapinduzi ingawa serikali na jeshi walikanusha taarifa hizo.
Wachambuzi wanasema licha ya serikali kudai rasmi kuwa hakukuwa na jaribio lolote la mapinduzi, lakini kunaashiria pengo katika ujasusi.
Chanzo: Dw