Afrika Kusini, mfanyakazi mmoja amekiri kuwalisha nguruwe miili ya binadamu baada ya kuamuliwa na Bosi wake afanye kitendo hicho.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari Bbc, Adrian De Wet (21) anadai aliambiwa atupe miili hiyo kwenye zizi la nguruwe kwani wanyama hao wanapokuwa na njaa ya kutosha hula chochote.
Akiendelea kuieleza mahakama, Adrian alikiri kuamuliwa kuwapiga risasi wanawake wawili na mmiliki wa shamba analofanyia kazi.
Bw Oliver ambaye ni mmiliki wa shamba na William Msora, wanatuhumiwa kwa mauaji ya Maria Makgato (45) na Lucia Ndlovu (34) wanaodaiwa walikuwa wanatafuta chakula kwenye shamba huko Limpopo ambapo Wet aliiambia Mahakama ya Polokwame kwamba yeye na Bosi wake walikuwa wanajihami baada ya wawili hao kuvuka mpaka Agosti,2024.
Wet, Alishitakiwa kwa mauaji lakini mahakama ilitupilia mbali baada ya Wet, kugeuka kuwa shahidi wa serikali.
Zaidi, Kesi hiyo imezua gunzo Afrika Kusini, na kuzidisha mvutano kuhusu ubaguzi wa rangi kati ya watu weusi na weupe nchini humo. Hali hii imeenea sana katika maeneo ya vijijini nchini humo, licha ya kumalizika kwa mfumo wa ubaguzi wa rangi miaka 30 iliyopita.
Chanzo: Tanzania Journal