Ripoti mpya iliyotolewa na mashirika kadhaa ya wanaharakati imetahadharisha kuwa mapambano dhidi ya malaria yamekwama licha ya miongo miwili ya mafanikio. Muungano wa Viongozi wa Afrika dhidi ya Malaria (ALMA) na mashirika mengine yameeleza katika ripoti hiyo kuwa athari za kuzuka upya maambukizi ya ugonjwa huu zitashuhudiwa zaidi barani Afrika ambako kunaripotiwa asilimia 95 ya visa vya ugonjwa wa Malaria ambao ulisababisha vifo 590,000 kote duniani mnamo mwaka 2023.
Ripoti hiyo imesema. ukosefu wa fedha za kutosha kwa ajili ya mipango yenye gharama kubwa ya kuzuia kuenea kwa malaria, unahatarisha juhudi dhidi ya ugonjwa huo unaoenezwa na mbu na hivyo kuyaweka hatarini maisha ya mamia kwa maelfu ya watu.
Chanzo: Dw