Wizara ya mambo ya nje ya Kenya imesema kuwa baadhi ya Wakenya wamekuwa wakishawishiwa ili kwenda kupigana upande wa Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine.
Katika taarifa iliyosainiwa na waziri wa mambo ya nje wa Kenya Musalia Mudavadi, imebainisha kwamba Wakenya wengi wameishia kuzuiliwa katika kambi za kijeshi nchini Urusi.
Taarifa hiyo imeongeza kwamba vitendo hivyo vinaendeshwa na mawakala na mafisadi ambao wanadai kufanya kazi na serikali na kuwalaghai Wakenya, wanaosafiri hadi Urusi na bila kujua wanajikuta katika operesheni za kijeshi za nchi hiyo.
Serikali ya Kenya imewataka raia kuwa waangalifu na kutotegemea ahadi za ajira kutoka kwa watu au mashirika yasiyo rasmi, hasa yanayodai kuwa na uhusiano na serikali au mashirika ya kimataifa.
Chanzo; Dw