Marekani inashirikiana na mataifa mengine kusitisha mapigano yanayoendelea nchini Sudan.
Hii ni kwa mujibu wa ikulu ya White House ijnayosema hatua hiyo imetokana na ripoti za mauaji makubwa baada ya wanamgambo wa RSF kuuteka mji wa el-Fasher wiki iliyopita.
Na sasa msemaji wa White House Karoline Leavitt amesema Marekani inafanya mazungumzo na Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri na Saudi Arabia kujaribu kuutatua mzozo huo ingawa amekiri kuwa si jambo rahisi.
Hayo yanafanyika wakati ambapo Sudan imesema kuwa jeshi lake litaendelea kupambana na wanamgambo wa RSF.
Baraza la usalama na ulinzi la Sudan limeyasema haya huku likiendelea kujadili pendekezo la Marekani la kusitishwa mapigano.
Huku hayo yakijiri wachambuzi wa kimataifa wa usalama wa chakula wanasema hakuna msaada wa chakula ulioingia nchini Sudan mwezi huu licha ya ripoti kuwa nchi hiyo inakabiliwa na njaa.
Chanzo; Dw