Mashirika ya kiraia yanakadiriwa kuwa chanzo cha ajali hiyo iliyosababisha hasara ya mali huenda ikawa ni umeme na ujenzi holela wa makazi.
Ajali hiyo ikiwa ni mfululizo wa ajali zingine za moto imetokea usiku wa kuamkia leo katika mji wa Bukavu jimboni Kivu Kusini.
Katika ajali hiyo nyumba nane zimeripotiowa kuteketea kwa moto na watu waliopoteza maisha ni wa familia mbili tofauti.
Mashirika ya kiraia yanakadiria kuwa zaidi ya visa ishirini vya moto vimerekodiwa katika miezi minne iliyopita katika mji wa Bukavu.
Chanzo: Dw