“Nilionekana kama mzigo wa kifedha kila wakati.” Hayo ni maneno ya msanii maarufu wa Nigeria, Tiwa Savage, akielezea changamoto alizokumbana nazo alipoingia katika tasnia ya muziki iliyotawaliwa na wanaume.
Tiwa anasema mahitaji ya msingi kama mtu wa kumpodoa, msusi, muda wa ziada wa kujiandaa au hata chumba kikubwa yalitafsiriwa kama gharama zisizo za lazima, jambo lililosababisha baadhi ya fursa kumfungia milango.
Lakini je, hali kama hii bado inawakumba wanawake wengi katika tasnia ya muziki barani Afrika? Na wadau wa muziki wanaweza kufanya nini kuhakikisha wanawake wanapata fursa sawa za kukuza vipaji vyao na kufanikiwa?