Mtengenezaji maudhui nchini Vicent Njau 'Kiredio'ambaye kwa sasa yupo Dubai, ameeleza hali ilivyo huku akisimulia wanavyoishi kwa sasa.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Kiredio amesema hali ni shwari. Kwasasa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
"Mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi, tupo salama na tupo Dubai mjini kabisa maana wapo waliosema tupo vijijini. Huku wanamfumo wa anga ambao ukitupa bomu linalipuka angani kabla halijatua ardhini. Nadhani mpaka jana ni zaidi ya mabomu 198 waliripoti yalitatuliwa angani.
"Jana Mfalme na Rais wa hapa walienda kutembea Dubai Mall kuonesha watu kwamba hali ni salama kabisa. Video nyingi ambazo zinaonekana mitandaoni sio za Dubai ulinzi wa hapa ni mzuri sana sehemu ambazo zilishambuliwa ni ile juzi tu Airport na zile kambi za Wamarekani,"amesema Kiredio
Utaumbuka hayo yote ni kufuatia mashambulizi yanayoendelea kati ya Israel na Marekani dhidi ya Iran. Mashambulizi hayo yaliyopelekea kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi mkuu wa Iran Ayatolaah Ali Khamenei pamoja na viongozi wengine wa nchi hiyo.
Chanzo; Mwananchi Scoop