Mtengenezaji maudhui na mchekeshaji maarufu kutoka nchini Jay Mondy ameweka rekodi nyingine hii ni baada ya kuwa Mtanzania wa kwanza kupata zaidi ya watazamaji bilioni 10 kupitia mtandao wake wa YouTube.
Jay anakuwa Mtanzani pekee na wakawanza kuweka rekodi hiyo ya kufikishi watazamaji bilioni 10 huku akimpiku nguli wa Bongo Fleva Diamond Plutnumz ambaye mpaka kufikia sasa anazaidi ya watazamaji bilioni 3 katika YouTube yake.
Aidha, Jay amefanikiwa kuvutia watazamaji wengi kupitia maudhui ya kucheza (dance) anayofanya pamoja na mpenzi wake wakiwa katika nchi mbalimbali. Kwenye video hizo fupi, huonekana wakicheza na mara nyingi hupata zaidi ya watazamaji milioni moja.
Hadi sasa amezunguka katika mataifa kama Uganda, Kenya, South Africa, France, Denmark, Singapore, India, Morocco, Finland na mataifa mengine mengi.
Utakumbuka mwaka 2024 mtengeneza maudhui huyo alipostiwa katika ukurasa rasmi wa Instagram wa YouTube kwa kuwa miongoni mwa madansa waliofanya vizuri kwenye 'chalenji' ya wimbo wa Tyla uitwao Art. Hatua hiyo ilipelekea Jay kuwa dansa pekee kutoka Afrika Mashariki kuwahi kupostiwa katika ukurasa huo.
Jay Mondy alianza sanaa akiwa kama mchekeshaji wa kuposti video kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii pamoja na kusimama katika majukwaa ya uchekeshaji ‘Starndup Comedy’ rasmi alianza kujikita katika dansi mwaka 2020 akiwa na mpenzi wake Isabell.
Kwasasa wapenzi hao wawili wanazunguka wakipita katika mataifa mbalimbali kwa ajili ya kufanya challenge za dance ambazo zimekuwa zikipokea maoni mazuri kutoka kwa mashabiki pande zote za dunia wanaowafuatilia.
Chanzo: Mwananchi Scoop