Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Joel Lwaga aelezea kwa kina sababu zinazomfanya au zitakazofanya asiwe mchungaji hapo mbele.
Kwenye mahojiano na Dozen Selection na mtangazaji maarufu wa Radio Hamis Mandi maarufu Bdozen, Joel Lwaga ameonyesha namna kazi hiyo inavyohitaji uvumilivu na kujitoa.
“Uchungaji hapa sijioni huko kwa sababu na amini kwenye nilichopewa, kuimba, lakini uchungaji una mambo mengi. Mimi ni muhubiri huwa siposti mambo yanayo husiana na upande huo lakini uchungaji ni zaidi ya kuhubiri.” Anaeleza Joel Lwaga.
“Uchungaji unabeba mambo mengi, jambo la kwanza, ni kitu ambacho Mungu anakuamini kuhusiana na roho za watu maelfu na mamia ya watu uwachunge na unahitaji kuwalisha neno kila siku.”
“Ni kazi ambayo inahitaji ujitoe kweli, cha pili, unachunga watu wa aina tofauti tofauti mimi nipo strict “Nimenyoka” unahitaji ujitoe.” Joel Lwaga
Anaendelea kwa kuelezea kwanini hajioni kuwa mchungaji hapo badae..
“Mchungaji unapaswa uwe na kifua, wanatunza vitu vya watu vizito
Msanii hiyo akaenda mbali kwa kuelezea kwanini Wachungaji wengi wanaonekana watoto wao wamewashinda au wasumbufu…
“Muda mwingi wa maisha ya wachungaji wanayatumia kwa maisha ya watu wengine wakati mwingine wanakosa muda na watoto wao.” Anamaliza Joel Lwaga.
Chanzo: Tanzania Journal