Mshindi wa Miss Universe Tanzania 2025, Naisae Yona, leo Oktoba 22 amekabidhiwa rasmi zawadi yake ya gari jipya aina ya Hyundai Creta katika hafla fupi iliyofanyika Jijini Dar es salaam,
Naisae baada ya kushinda taji hilo August 24 mwaka huu alipewa zawadi ya shilingi milioni 10 pamoja na gari hili ambalo amekabidhiwa rasmi leo ambapo sasa kilichobaki ni kuipeperusha bendera ya Tanzania mashindano ya Dunia ya Miss Universe yatayofanyika Novemba 21 mwaka huu Nchini Thailand.
Naisae Yona aliibuka Mshindi wa Miss Universe Tanzania miongoni mwa Warembo 35 kutoka Mikoa sita Nchini ambayo Dar es salaam, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Arusha na Visiwa vya Zanzibar waliojitosa kuwania taji la Miss Universe Tanzania 2025.
Chanzo: Millard Ayo