Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

P Diddy Kuachiwa 2028

Mwanamuziki na mfanyabiashara maarufu kutoka Marekani, Sean “Diddy” Combs, anatarajiwa kuachiwa huru kutoka gerezani Mei 8, 2028, baada ya kutumikia sehemu ya kifungo chake cha miaka minne na miezi miwili.

Diddy, ambaye alikamatwa Septemba 2024, Oktoba 3,2025 alihukumiwa na mahakama ya New York kwa makosa mawili ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ukahaba huku mashtaka makubwa ya sex trafficking na racketeering yakitupiliwa mbali.

Jaji Arun Subramanian alitoa hukumu hiyo, sambamba na faini ya dola 500,000 na masharti ya kifungo cha nje kwa miaka mitano baada ya kuachiwa huru.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ‘Federal Bureau of Prisons’, Diddy amekuwa akitumikia kifungo chake katika gereza la Metropolitan Detention Center jijini Brooklyn, tangu kukamatwa kwake huku akitarajiwa kuachiwa Mei 2028 kutokana na kupunguziwa muda wa kukaa gerezani inayojuliakana kama ‘Good Conduct Time’.

Hata hivyo vyanzo vya karibu na gereza hilo vimeeleza kuwa Diddy anaweza kuachiliwa mapema zaidi endapo atajiunga na ‘Residential Drug Abuse Program (RDAP)’ shirika linalosaidia kupunguza muda wa kifungo kwa mtuhumiwa ambapo shirika hilo linaweza kumpunguza kifungo muhusika hadi miezi 12.\

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: