Jake Paul atakua na kipindi cha miezi tisa cha uangalizi kiafya baada ya Anthony Joshua kuvunja taya yake wakati wa pambano lao.
Hata hivyo, kutokana na mvunjiko huo wa taya kupita kwenye mizizi ya meno ya Paul, atahitaji kuwekwa vipandikizi vya meno, ambapo utaratibu huu unatarajiwa kufanyika takribani miezi mitatu baada ya mvunjiko huo kupona.
Paul huenda akahitaji pia kuwekwa waya kwenye meno - mchakato ambao kawaida unachukua miezi sita hadi saba zaidi - hivyo inaweza kuchukua angalau miezi tisa kabla ya mchezaji huyo kurejesha nguvu za taya yake kwa asilimia 90.
Chanzo; Bongo 5