Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Harmonize Apenya Grammy na Nyimbo Nne

Nyimbo nne alizoshiriki mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize rasmi zimeingia na kutambuliwa na Grammy Academy kwa ajili ya hatua ya kwanza ya mchujo 'Consideration' katika kinyang'anyiro cha tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika Februari 1, 2026.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii mwanamuziki huyo ameonesha furaha yake kuingiza nyimbo nne katika hatua hiyo. Nyimbo hizo ni pamoja na Me Too ft Abigail Chams, Simuoni aliyoshirikishwa na Ay, Furaha, na Finally aliyomshirikisha Miri Ben-Ari. Nyimbo zote nne zimewasilishwa kwenye Kipengele cha Best African Music Perfomance.

Utakumbuka kwenye hatua hiyo Harmonize ameingia na msanii wa Hip hop Fid Q ambaye ameandika historia hiyo mpya baada ya wimbo wake unaopatikana kwenye albamu yake ya Kitaa Rejex iliyotoka 2025, Glory 2 aliomshirikisha Damian Soul na Jose Chameleone kuingizwa katika mchujo wa Tuzo za Grammy.

Pia, nyimbo mbili za mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, Ay zimeidhinishwa na kupitishwa rasmi na Grammy Academy kwa ajili ya mchakato unaofuata wa kuteuliwa kwenye vipengele vya tuzo hizo. Nyimbo za Ay zilizofanikiwa kupenya kwenye hatua hiyo ni Simuoni aliyomshirikisha Harmonize, na Wanganeka ft Kanjiba.

Baada ya hatua hiyo nyimbo zilizofanikiwa kupenya kwenye Consideration ya Grammy zinapigiwa kura na kamati ya Grammy Academy kwaajili ya kuingia kwenye vipengele 'Nomination' za tuzo hizo. Upigaji wa kura ulianza Oktoba 3, na utamalizika Oktaba 15, 2025, nyimbo na wasanii watakaowania vipengele vya tuzo hizo watatangazwa Novemba 7, 2025, wakati tuzo za 68th za Grammy zinatafanyika Februari 1, 2026.

 

Chanzo: Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: