Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Gonjwa la Koo Lashambulia Sauti ya Selena Gomez

Mwimbaji wa Pop kutokea Marekani, Selena Gomez, 33, hatimaye ameweka wazi sababu ya mabadiliko ya sauti yake ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakizua mijadala miongoni mwa mashabiki wake.

Selena, mkali wa kibao cha Calm Down (2022), akizungumza kupitia Insta Live, alijibu swali la shabiki aliyekuwa akitaka kujua kwanini sauti yake imekuwa tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Akijibu swali hilo, Selena alisema mabadiliko hayo ya sauti wanatokana na hali yake ya kiafya kwa sasa huku akisisitiza kuwa hajali sana maoni hasi ya watu kuhusu hali hiyo.

"Wakati mwingine mambo hutokea. Koo langu huwa linavimba kwa ndani mara nyingine, na hilo ndilo linalosababisha mabadiliko ya sauti," alisema Selena.

Mara kadhaa amekuwa wazi kuhusu changamoto zake za kiafya, hasa ugonjwa wa Lupus ambao unaweza kusababisha uvimbe unaoathiri viungo mbalimbali vya mwili, ikiwemo koo na mapafu, hali inayoweza kuathiri sauti.

Baada ya kauli hiyo, mashabiki walitoa maoni yao kwenye mitandao wakimsifu kwa ujasiri na uaminifu wake. Wengi walieleza kumuunga mkono na kumpongeza kwa kuzungumza wazi kuhusu hali yake bila aibu.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: