MTV, chaneli maarufu ya kimuziki iliyobadilisha kabisa tasnia ya muziki tangu ilipoanzishwa mwaka 1981, yatangaza kufunga shughuli zake baada ya kuzitumikia kwa miaka 44.
Sababu inatajwa kuwa, Watazamaji wameacha kutazama muziki kwenye TV. Ugunduzi umehamia YouTube, TikTok, Instagram, na majukwaa ya kutiririsha muda mrefu uliopita, na kuacha chaneli za muziki za kitamaduni nyuma.
Kwa miongo kadhaa, MTV haikuonyesha video za muziki, bali ilikuwa jukwaa la kitamaduni lililobainisha vizazi, likiwasukuma wasanii na aina mpya za muziki kuwa klassiki za milele.
Athari ya MTV katika muziki ilikuwa kubwa, ilisaidia kueneza aina mpya za muziki, kuwapa wasanii umaarufu wa kimataifa, na kubadilisha jinsi watazamaji walivyotumia muziki . Mtindo wake wa ubunifu uliunda daraja kati ya muziki na media, na kuacha urithi usiosahaulika katika tasnia hii ya habari hasa za kiburudani.
Ingawa habari hii inaweza kuwa ya kusikitisha kwa wengi wetu ambao tulikua tukitazama video za muziki bila kukoma, urithi wa MTV utaendelea kuishi kupitia nyimbo, wasanii na kumbukumbu ambazo ilituachia. Asante MTV kwa miaka yote ya burudani na mapinduzi!
Chanzo: Tanzania Journal