“Lisemwalo lipo na kama halipo laja, kwani sina haki ya kubeba ujauzito jamani? Tena nafurahia kumzalia Aziz KI mume wangu wa ndoa.” Haya ni maneno ya mrembo Hamisa Mobetto ambaye ni mke wa nyota wa zamani wa Yanga na kwa sasa anakipiga Wydad AC, Stephanie Aziz KI.
Kama hujui hili, basi jua kupitia Mwananchi Scoop kuwa, habari ya mjini kwasasa ni Hamisa anadaiwa kunasa ujauzito hivyo yupo mbioni kutimiza ndoto yake ya kupata mtoto wa tatu hivi karibuni.
Hamisa ameibua gumzo mitandaoni kufuatia muonekano wake wa sasa, baada ya kutupia picha mtandaoni ambayo iliwafanya wajuzi wa mambo kuikagua vilivyo na kuhitimisha kuwa ni mjamzito.
Chanzo; Mwananchi Scoop