Mfanyabiashara na mwanamitindo maarufu kutoka Marekani, Kim Kardashian ameweka wazi kuwa anafikiria kuachana na masuala ya umaarufu ili aweze kugeukia kwenye kazi yake aliyosomea ya Uwakili.
Akiwa kwenye kipindi cha ‘The Graham Norton Show cha BBC’, Kim alionekana mwenye furaha na kujiamini akisema kuwa amebakiza wiki mbili tu kumaliza masomo yake ya sheria, na ndoto yake kubwa ni kusimama mahakamani kama wakili wa kweli.
“Nina miradi kadhaa inayonisubiri. Nitakuwa nimehitimu rasmi wiki mbili zijazo. Nataka kufanya kazi kama wakili, na labda baada ya miaka 10 nitaacha kabisa kuwa Kim K wa umaarufu, niwe wakili wa kesi mahakamani,” amesema Kim
Aidha mbali na hilo ameeleza kuwa ifikapo mwezi Januari anampango wa kurekodi filamu yake ya kwanza lakini pia anampango wa kuachia msimu wa pili wa All’s Fair.
Chanzo: Mwananchi Scoop