Msanii wa Bongo Fleva Rashid Makwiro almaarufu Chid Benz anasema kwasababu yeye kama msanii ni wa jamii yote hivyo licha ya kutafutwa na vyama mbalimbali vya siasa lakini amekuwa akikataa mialiko hiyo.
Chidi Benz anasema kuwa “Natamani hizo pesa lakini naangalia, watu wananiuliza. Sijawahi kitu chochote cha kuhusiana na Chama.”
“Nimepigiwa na vyama vitatu kwenda kufanya matamasha, sijawahi kukubaliana nao chochote naogopa nionekane nimebagua.” - Chidi Benzi
Chidi Benz amerejea kutoka nyumba ya nafuu ‘Sober House’ siku za hivi karibuni na ameonekana kuimarika kiafya na sasa anajidhatiti kurejea tena kwenye muziki kwa kishindo kama ilvyokua awali alipokua akitamba na vibao kama ngoma itambae na mashallaah.
Chanzo: Bbc