Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Ataka Kukwepa Bili kwa Kujifanya Mke wa Eminem

Mwanamke mmoja aitwaye Jennifer Kleber kutoka Florida Marekani mwenye umri wa miaka 54, amekamatwa na polisi baada ya kujitambulisha kuwa ni mke wa rapa Eminem.

Inaelezwa kuwa Kleber aliingia katika mgahawa uitwao Darrell’s Dog Gone Good Diner na kula chakula chenye thamani ya dola 27.55 na baada ya kumaliza kula alikataa kulipa akidai kuwa hana pesa, lakini akasisitiza kuwa mume wake Eminem ndiye atalipa bili hiyo kwa sababu ana pesa nyingi sana.

Baada ya kuhojiwa aliendelea kusisitiza kuwa yeye ni mke halali wa rapa maarufu Eminem jambo ambalo liliwashangaza wahudumu wote ndipo kuchukua jukumu la kuita polisi kwa ajili ya kumkamata.

Hata hivyo meneja wa mgahawa alisema si mara ya kwanza kwa mwanamke huyo kutembelea eneo hilo na kuondoka bila kulipa, lakini safari hii alikuja na kisingizio kipya cha kudai kuwa ni mke wa nyota huyo mkubwa wa muziki. Polisi walipofika, walimkamata kwa kosa la udanganyifu na kumpeleka kituoni kwa mahojiano zaidi.

Aidha taarifa zinasema hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kwamba Kleber ana uhusiano wowote na Eminem, hivyo alifanya udanganyifu kwa lengo la kujipatia chakula.

 

Chanzo: Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: