Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Michaele Jackson Alivyovaa Abaya kuwakwepa Mashabiki, Paparazi

Baada ya kupitia moja ya kesi kubwa zaidi katika maisha yake, mwaka 2005 marehemu staa wa muziki duniani Michael Jackson aliamua kuondoka kabisa Marekani na kuelekea Bahrain, taifa dogo lililoko Ghuba ya Uajemi.

Kutokana na kesi hiyo inaelezwa msanii huyo alichukua uamuzi wa kuvaa Abaya pamoja na Nikabu ili kuepuka mashabiki na paparazi waliokuwa wakimuandama. Kesi hiyo ni ile iliyomuhusisha kijana mmoja aliyedai MJ alimnyanyasa kingono akiwa katika makazi yake huko Neverland Ranch.

Kwa miezi kadhaa, mashahidi mbalimbali walitoa ushahidi huku vyombo vya habari vikimfuatilia msanii huyo kila hatua. Lakini Juni 2005, majaji walimkuta hana hatia katika mashitaka yote na kufutiwa kabisa mashtaka hayo.

Aidha baada ya kuumizwa na kitendo hicho watu wa karibu wa MJ wanaeleza msanii huyo alikata tamaa ya kuishi Marekani ndipo akaamua kupokea mwaliko wa muda mrefu kutoka kwa Sheikh Abdulla bin Hamad Al-Khalifa, mwana wa mfalme wa Bahrain, ambaye alikuwa shabiki yake mkubwa.

Mwanamfalme huyo alimpa hifadhi, nyumba ya kifahari na faragha msanii huyo aliamua kuishi maisha yake huku mara nyingi akionekana anatembelea maduka makubwa akiwa amevalia Abaya na Nikabu ili kuficha uso wake.

Vazi hilo kwa kawaida ni marufuku kuvaliwa na wanaume katika nchi za Kiarabu, lakini kwa sababu alikuwa chini ya ulinzi wa kifalme, hakukamatwa wala kuhojiwa.

 

Chanzo: Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: