Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wiz Khalifa Jela Miezi 9 kwa Kuvuta Bangi Jukwaani

Rapa wa Marekani Wiz Khalifa amehukumiwa kifungo cha miezi tisa jela nchini Romania baada ya kushtakiwa kwa kuvuta bangi jukwaani wakati wa tamasha lake.

Tukio lilitokea Julai 2024 wakati alipokuwa akitumbuiza katika tamasha la Beach, Please! huko Costinești, ambapo polisi walimkamata na kukumkuta na zaidi ya gramu 18 za bangi, pamoja na kuvuta moja kwa moja jukwaani.

Awali, mahakama ya chini ilimtoza faini ya takriban lei 3,600 (karibu dola 830 za Marekani), lakini waendesha mashtaka walikata rufaa na kushinda, hivyo mahakama ya rufaa ya Constanța ikatoa hukumu hii ya kifungo cha miezi tisa kwa makosa ya "kumiliki dawa hatari bila ruhusa kwa matumizi ya kibinafsi".

Romania ina sheria kali sana kuhusu dawa za kulevya, ambapo bangi ni haramu kabisa, na kumiliki kwa matumizi binafsi kunaweza kutoa adhabu ya kifungo cha miezi 3 hadi miaka 2 au faini.

Timu ya kisheria ya Wiz Khalifa inatarajiwa kukata rufaa dhidi ya hukumu hii, na bado haijulikani wazi kama atatumikia kifungo hicho, hasa kwa kuwa yeye ni raia wa Marekani na kwa sasa yuko nchini Marekani. Wataalamu wanasema uwezekano wa kumrejesha Romania kwa nguvu (extradition) ni mdogo sana kutokana na hali ya kisheria ya bangi Marekani.

Wiz Khalifa, ambaye jina lake halisi ni Cameron Jibril Thomaz, alishajiweka wazi kuhusu matumizi ya bangi, pia ana brand yake mwenyewe ya Khalifa Kush. Baada ya tukio la awali, aliomba radhi kwenye mitandao, akisema hakuwa na nia ya kuidharau Romania.

 

Chanzo; Tanzania Journal

Kuhusiana na mada hii: