1. Diamond Platnumz
Msanii na mfanyabiashara na CEO wa WCB Lebo pamoja na Wasafi media, amefanikiwa kuingia kwenye mchakato wa tuzo za muziki wa Grammy kupitia ngoma yake aliyoshirikishwa na Ciara inayokwenda kwa jina la “Low” inayopatikana kwenye Ep ya “Cici” yake Ciara. Wimbo huo umewasilishwa kwenye vipengere viwili Best Music Video pamoja na Best African Music Video.
2. Harmonize
Msanii pekee Toka Tanzania ambaye nyimbo nne zenye sauti yake zimefanikiwa kuwasilishwa kwenye mchakato wa nyimbo zitakazo penya kwenye vipengere vya kuwania tuzo hizo 2026, Furaha, Finally aliyomshirikiana na Miri Ben, Simuoni aliyoshirikishwa na Ay pamoja Me too aliyoshirikiana na Abigail Chams ambapo zote zipo kwenye kipengere cha Best African Music Perfomance.
3. Ay
Moja ya wasanii wa Rap aliyefanikisha kupenyezesha nyimbo mbili kwenye mchakato wa ngoma zitakazo shiriki kwenye Grammy ya 68. Simoni aliyomshirikisha Harmonize katika kipengere cha Best African Music Perfomance na Wangeneka aliyomshirikisha Kanjiba.
4. Fid Q
Akiwa anaifunga orodha ya marapa wawili toka Tanzania kuingiza nyimbo zao kwenye mchato wa awali wa uwasilishaji, mwanahiphop huyo amefanikiwa kuwasilisha wimbo wa “Glory 2” Ft Damian Soul na Chameleon toka Uganda, kwenye kipengere cha Best African Music Perfomance.
5. Abigail Chams
Mwanamke pekee toka Tanzania kuwasilisha ngoma yake Grammy, Me too, aliyoshirikiana na Harmonize ndio wimbo amefanikisha kuuwasilisha katika kipengere cha Best African Music Perfomance.
Ikumbukwe, Tuzo hizo zitafanyika Februari,2026 na zitakuwa tuzo za 68 tangu Tuzo hizo zianzishwe, na kuufanya mwaka 2025 kuwa mwaka wa neema kwa Bongo Fleva kwa wasanii wengi karibu wa wato kushiriki mchakato wa grammy kwa wakati mmoja. Pamoja na hayo swali kubwa wa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva ni nani kuileta Grammy kwa mara ya kwanza Tanzania ?
Chanzo: Tanzania Journal