Katika habari ambazo zimetingisha ulimwengu wa soka na filamu Disemba,2026, nyota wa soka wa kimataifa Cristiano Ronaldo, ameonekana kwenye baadhi ya vipande vya filamu ya Fast X: Part 2 au Fast & Furious 11, ambayo inatarajiwa kuwa mwisho kwenye mlolongo wa uachiaji wa kazi hizo, ambayo itaachiwa Januari,2027.

Vin Diesel, staa na mtayarishaji mkuu wa filamu hiyo, alichapisha picha yake na Ronaldo kwenye Instagram Disemba 12, akiandika: "Kila mtu amekuwa akiuliza kama atakuwa kwenye Fast mythology... Lazima niwaambie, yeye ni wa kweli. Tumeandika kazi yake..." Hii ilithibitisha kuwa wameandika nafasi maalum kwa Ronaldo, na inaonekana kuwa sehemu ndogo lakini ya maana.
Kisha, Tyrese Gibson (anayecheza Roman Pearce) alichapisha picha ya kundi la waigizaji – ikiwa na Ronaldo katikati – pamoja na Vin Diesel, Dwayne "The Rock" Johnson, Jason Statham, Michelle Rodriguez, Ludacris na wengine. Aliongeza caption: "Welcome to the FAMILY! Cristiano... The global dance just went into new heights!" Picha hii ilionekana kama ilipigwa kwenye seti, na magari ya michezo nyuma, ikionyesha Ronaldo akicheka na kufurahia na "Fast Family".
Ingawa baadhi ya maoni ya watu wana shaka kama picha za hivi karibu ambazo ameonekani kama akiigiza wakidai ni AI-generated, maoni mengi kutoka waigizaji yenyewe yanaonyesha kuwa Ronaldo amejiunga rasmi na cast. Filamu hii, inayoongozwa na Louis Leterrier, inatarajiwa kutolewa Aprili 2027.
Licha ya yote filamu hii itashanga Ulimwengu wa Soka na Filamu Namna Gani ?
1. Crossover Kubwa Zaidi Kati ya Sports na Hollywood: Ronaldo, mwenye wafuasi zaidi ya bilioni kwenye mitandao, anapofanya acting debut au cameo katika franchise yenye mafanikio makubwa kama Fast & Furious (ambayo imepata mabilioni ya dola), itavuta mashabiki wa soka na filamu kwa pamoja. Hii inaweza kuwa moja ya crossovers zenye nguvu zaidi tangu wakati wa nyota kama The Rock au John Cena walipoingia filamu.
2. Kuongeza Umaarufu wa Filamu: Fast saga imekuwa ikiongeza nyota wa kimataifa (kama Jason Momoa, Charlize Theron), lakini Ronaldo ataleta watazamaji wapya kutoka Ulaya, Asia na Amerika Kusini ambapo soka ni dini. Hii inaweza kufanya filamu hii kuwa moja ya zenye mapato makubwa zaidi, hasa ikizingatiwa kuwa ni finale.
3. Maisha ya njee ya Soka kwa Ronaldo: Akiwa na umri wa miaka 40 na bado anacheza Al-Nassr na Portugal, tayari ana studio yake ya filamu na Matthew Vaughn.
4. Mitandao na Buzz: Tayari habari hii imesambaa kila mahali kutoka Reddit hadi X (Twitter) na AI images za Ronaldo akifanya action scenes zimeanza kuenea. Wakati trailer au clips zitakapotoka, itakuwa viral zaidi, na labda kuwafanya mashabiki wa Messi na Ronaldo kugombana tena kuhusu nani bora hata kwenye screen!
Chanzo: Tanzania Journal