Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wema Amejaa kwa Pacome

Msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu amekumbuka makubwa aliyofanyiwa na mashabiki wake mwaka 2022 ukiwamo upendo waliomwonyesha akiwa katika wakati mgumu na kukiri ameyaandika kwenye kitabu chake cha kumbukumbu.

Wema anasema moja kati ya mambo hayo ni kitendo cha mashabiki wake kuonyesha wako naye pamoja hata baada ya kushambuliwa na mfanyabiashara maarufu mitandaoni, Aristote aliyedai hana gari zuri la kifahari kama ilivyo kwa Irene Uwoya, kauli iliyopokelewa kwa hisia kali na wengi hadi Aristote mwenyewe kuomba radhi.

Wema ambaye aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006, anasema kati ya vitu ambavyo hawezi kuvisahau kwa mashabiki zake, ni kitendo cha kuamua kumchangia pesa ili anunue gari ingawa hajawahi kuwaomba mchango. Pia amefunguka kuhusu sherehe yake ya siku ya kuzaliwa na jinsi nyota wa Yanga, Pacome Zouzoua anavyomchanganya kutokana na mavitu yake.

“Nakumbuka ilikuwa mwaka 2022 na huwezi amini nimeandika kwenye kitabu changu cha kumbukumbu, mimi binafsi sikuwahi kumwambia mtu yeyote anichangie pesa. Nadhani ilikuwa ni upendo na watu wakaamua kuchanga, lakini niliwaambia siko tayari kukubaliana na hicho kitendo chao na wasitishe hilo zoezi na walisitisha. Sasa kwa kitendo hiki huwa nawathamini na kuwapenda sana mashabiki zangu, yaani huwa wanalia na mimi na kucheka na mimi ndiyo maana nawaheshimu sana.

“Chaguo langu ni Pacome Zouzoua, wapo wachezaji wengi na wanacheza vizuri ila kwa huyu Pacome bado yuko kichwani mwangu. Siwezi taja majina ya timu yote sababu siwafuatilii sana, ila ukiniuliza mchezaji gani ananikosha akiwa uwanjani nitakwambia Pacome kwa sababu napenda anavyojituma uwanjani, yaani anapambana, pia anamuonekano mzuri hata akiwa nje ya uwanja, ukimuangalia tu, unasema yes! huyu ni bonge la mpambanaji,” amesema

 

Chanzo: Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: