Rapper Sean John Combs ‘Diddy’ wa Marekani, ataachiliwa huru kutoka Gerezani mwezi mmoja na nusu mapema zaidi ya tarehe iliyokuwa imepangwa hapo awali ambapo badala ya kutoka June 4, 2028 sasa ataachiwa huru Aprili 25, 2028.
Hii si mara ya kwanza kubalishwa kwa tarehe ya kutolewa kwa Staa huyu ambaye anatumikia kifungo chake katika Gereza la Fort Dix huko New Jersey ambapo awali adhabu yake iliongezwa kutoka Mei 8, 2028 hadi Juni 4, 2028 mnamo mwezi Novemba 2025 baada ya Diddy kudaiwa kukiuka sheria nyingi za magereza ikiwemo madai ya kutumia simu za magendo kitendo ambacho ni marufuku.
Imeelezwa kuwa sababu ya kuachiliwa mapema kwa Staa huyu mwenye umri wa miaka 56 kwa sasa ni nidhamu yake baada ya kujiunga na programu ya matibabu ya utumiaji wa dawa za kulevya programu ambayo inaweza kupunguza muda wa kifungo kwa wale wanaoshiriki kikamilifu.
Diddy yuko Gerezani kutumikia kifungo cha miaka minne baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha Watu kushiriki katika shughuli za ngono ambapo alikamatwa Septemba 2024 na hukumu ikatolewa tarehe 3 Oktoba 2025.
Chanzo; Millard Ayo