Mwaka mmoja umepita tangu msanii Lil Durk akamatwe huko Broward, Frolida kwa mashtaka yanayohusiana na mauaji ya binamu wa msanii Quando Rondo, Saviay'a Robinson maarufu Lul Pab, mnamo Agosti 2022.
Lil Durk amekana shutuma na anasisitiza kuwa hana hatia. Kwa sasa msanii huyo yupo kizuizini Kituo cha Metropolitan huko Los Angeles, na kesi yake itaanza kusikilizwa Januari 6, 2026.
Visibitisho vitatu vilivyoanikwa kwa mujibu wa mashtaka ya shirikisho vinavyozidi kumuweka msanii huyo hatiani moja, Tiketi za ndege na hoteli zilizolipwa kwa kadi za mkopo zinazohusishwa na Lil Durk na OTF. Mbili, Ushuhuda wa mashahidi wasiotajwa majina wanasema Lil Durk aliahidi malipo. Tatu, Video za usimamizi zinazoonyesha wanaume hao wakilifaya gari la Quando Rondo.
Chanzo: Tanzania Journal