Dansa anayetikisa kupitia wimbo wa Mbosso Khan “Aviola”, Queen Fraison, amefunguka kuhusu kazi yake ya unenguaji ambayo kwa sasa ndiyo inampa zaidi kipato.
Queen Fraison amesema, hapendi kucheza hadharani au kujidhalilisha, lakini hana budi kuendelea nayo kwani ndiyo kazi inayomuweka mjini.
“Sipendi kucheza hadharani au kujidhalilisha, mimi nina familia na nina wazazi kama watu wengine, lakini sina jinsi kwa sababu hii ni kazi inayolipa na siwezi kuiacha, hata familia yangu pia inalijua hilo,” amesema.
Fraison ameeleza kuwa wengi hawajui umaarufu alioupata umetokana na sanaa ya kucheza, na kwa sasa amekuwa akipata mialiko mbalimbali ya maonyesho kupitia kipaji chake hicho.
Chanzo: Mwanaspoti