Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Chritian Bella Apewa Uraia wa Tanzania

Msanii maarufu wa muziki wa Bongofleva wenye ladha ya R&B na Afro-pop, Christian Bella amepewa uraia wa Tanzania.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene leo Alhamisi, Desemba 18, 2025 ikiwa ni siku ya wahamaji duniani.

Simbachawene amesema Tanzania kuna idadi kubwa ya wahamiaji na baadhi yao wamekuwa wakipewa uraia.

“Sasa anakwenda wapi, amekwisha fika, ameoa hapa, ana watoto hapa na atapata wajukuu hapa. Anafanya kazi vizuri, hana makosa, amefuata utaratibu na muda wote alioishi hapa amelipa malipo stahiki, siyo wengine wanaolanda landa tu,” amesema Simbachawene.

Amesema mtu anaweza kupewa uraia na ukafutwa kama hatafuata utaratibu: “Hatuwezi kumpa uraia mtu ambaye ni hatari ama anayegeuka kuwa hatari, kwa hiyo kuna ‘vetting’ imefanyika kabla ya mtu kupewa uraia.”

Awali, Bella alikuwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambaye ameishi Tanzania kwa muda mrefu akifanya shughuli za kisanii.

 

 

Channzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: