Msanii wa Tanzania Rayvanny ameendelea kuiwakilisha Tanzania kwenye jukwaa la kimataifa baada ya kutangazwa kuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza katika Afro Nation, tamasha kubwa la muziki wa Afrobeats na muziki wa Kiafrika.
Tangazo rasmi la awamu ya kwanza la tamasha hilo limetaja Rayvanny pamoja na majina makubwa kutoka Afrika na kimataifa, akiwemo Davido, Rema, Fally Ipupa, GIMS, Omah Lay, Shenseea, Victony, Valiant na wengine.
Rayvanny anakuwa miongoni mwa wawakilishi muhimu kutoka Tanzania kwenye tamasha hilo, ambalo linatarajiwa kufanyika 9–11 Juni 2027 katika Praia da Rocha, Portimão, Portugal.
Kwa upande wa mastaa wakubwa, Davido, Rema na Fally Ipupa wametajwa kuwa miongoni mwa vinara wa jukwaa kuu la LIT Stage, huku GIMS akiwa mgeni maalum.
RayVanny na Davido Uso kwa Uso
- Chanzo:
- Bongo 5