Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Watu 5000 Wacheza “Kalinka” Kuelekea Tamasha la Kimataifa la Vijana 2026

Kuelekea Tamasha la Kimataifa la Vijana 2026 litakalofanyika jiji la Ekaterinburg kuanzia Septemba 11 hadi 17, 2026, wafanyakazi 5,000 wa kampuni ya biashara na uzalishaji ya Sima-Land yenye makao yake makuu jijini humo, walishiriki katika tukio maalum la amsha amsha lililoambatana na wimbo maarufu wa Kirusi “Kalinka.” Kupitia tukio hilo, wafanyakazi wa kampuni hiyo walituma salamu za muziki kwa washiriki wa tamasha hilo ambao wanatarajiwa kukutana hivi karibuni katika Mji wa Vijana wa Dunia. Sima-Land ni kampuni kubwa zaidi ya biashara na uzalishaji nchini Urusi, ikiwa na takribani wafanyakazi 9,000, ambapo sehemu kubwa ni vijana. Makao makuu ya kampuni hiyo yako Ekaterinburg huku ikiwa na ofisi za uwakilishi katika maeneo mbalimbali ya Urusi na nje ya nchi. Tamasha la Kimataifa la Vijana 2026 linatarajiwa kuwakutanisha vijana 10,000 kutoka nchi 191 duniani ikiwemo Tanzania.

Kuhusiana na mada hii: