Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka amesema ushiriki wa vijana wa Tanzania katika Tamasha la Vijana nchini Urusi umewasaidia kupanua mitazamo yao na kutambua fursa mbalimbali ambazo awali walidhani hazikuwezekana.
Nanauka amesema kupitia tamasha hilo vijana hao wamepata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali, kubadilishana uzoefu na kuongeza ujuzi, jambo ambalo limewasaidia kuangalia fursa kwa mtazamo mpana zaidi.
Mwandishi wetu, @balqis_njuki, akiwa nchini Urusi katika Tamasha la Vijana, amefanya mazungumzo na Waziri Nanauka na kumuuliza kuhusu faida ambazo vijana wa Tanzania wamezipata kupitia ushiriki wao katika tamasha hilo.
Aidha, Waziri amesema vijana hao wamepata nafasi ya kukutana na vijana kutoka mataifa mbalimbali na kujenga mahusiano yatakayowawezesha kubadilishana maarifa na uzoefu katika maeneo mbalimbali.