Vikosi vya usalama nchini Uganda vimemuua mganga wa jadi, Christian Asuman Muganzi, anayedaiwa kuongoza mashambulizi ya kuratibiwa dhidi ya vituo vya polisi na jeshi katika wilaya za Bundibugyo, Kasese na Fort Portal, karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
Zaidi ya wapiganaji 20 waliuawa, wengine 15 wakakamatwa.
Mganga huyo alitumia eneo lake ya jadi kusajili na kuwalinda wapiganaji wake kwa kutumia dawa za mitishamba na imani za kishirikina.
Mashambulizi hayo yalilenga kuchukua silaha kwa ajili ya kuanzisha kikundi cha wanamgambo. Uganda bado inakabiliwa na vitisho kutoka kwa makundi ya waasi katika maeneo ya magharibi, hasa karibu na DRC.
Chanzo; Dw