Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Samia awaonya Wanaharakati

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaonya Watu wanaojiita Wanaharakati huku akisisitiza kuwa vitendo vyovyote vya ugaidi havitavumiliwa Nchini.

Akizungumza leo Julai 9, 2026 Zanzibar wakati wa hafla ya kushuhudia Tamko la Pamoja la Maridhiano ya Kisiasa na utiaji saini wa makubaliano kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo, Rais Samia amesema baadhi ya Watu hujisitiri kwa sura ya uzalendo na uanaharakati huku wakifuata maslahi yao binafsi.

“Nitumie fursa hii kuwaonya wote wanaojiita Wanaharakati ili watambulike duniani lakini matendo yao ni ya kigaidi,” amesema Rais Samia.

Ameongeza kuwa baadhi ya Watu au Makundi huonekana kuwa na sura ya kizalendo lakini ndani yake wakawa na maslahi binafsi ambayo hayaendani na ustawi wa Taifa.

“Watu wanavaa sura za uzalendo lakini ndani yake wana maslahi binafsi, nawasihi Watanzania tushikamane kwa maendeleo yetu na si kuwa kundi la watu fulani,” amesema.

Kuhusiana na mada hii: