Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Khamenei kuzikwa leo Mashhad, Iran

Maelfu ya Wananchi wa Iran leo Julai 9, 2026, wamekusanyika katika Mji Mtakatifu wa Mashhad kushiriki mazishi ya Kiongozi Mkuu wa Nchi hiyo, Ayatollah Ali Khamenei, aliyefariki dunia kufuatia shambulio la bomu lililotokea Februari 28, 2026.

Mazishi ya Khamenei yanafanyika katika eneo la Shrine of Imam Reza baada ya maombolezo yaliyodumu kwa takribani wiki moja na kupita katika Miji mitakatifu ya Najaf na Karbala Nchini Iraq kabla ya kuhitimishwa Mashhad, Mji aliozaliwa Kiongozi huyo.

Wakati Khamenei akizikwa, hatma ya mrithi wake na Kiongozi Mkuu mpya wa Iran, Mojtaba Khamenei imeendelea kuwa gumzo Nchini humo kutokana na kutokujitokeza hadharani tangu kuanza kwa vita vilivyosababisha kifo cha Baba yake, huku ripoti zikieleza kuwa bado hajajitokeza kwa sababu za kiusalama na afya.

Kuhusiana na mada hii: