Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Heche Asema Aliingia Bungeni Kwa Uchaguzi Wenye Figisu

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, inaendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam ambalo Heche anaendelea kuhojiwa maswali ya dodoso na wakili Katuga upande wa Jamhuri.

Wakili Katuga: Ulisema vyombo vya habari havitoi nafasi sawa kwa wagombea?

Heche: Ni sahihi.

Wakili Katuga: Uliiambia Mahakama mengi kuhusu mapungufu ya uchaguzi.

Heche: Sahihi.

Wakili Katuga: Ulieleza ni aina gani ya mfumo wa uchaguzi unazuia vyombo vya habari visitoe nafasi sawa?

Heche: Nilieleza.

Wakili Katuga: Ulieleza ni sheria ipi inayowaambia waandishi wa habari toeni habari hii na hii msitoe?

Heche: Kuna upendeleo.

Wakili Katuga: Umesema kutokana na kutokuwa na usawa wa sheria za uchaguzi, kwamba kuna sehemu mawakala wamekuwa wakipata usumbufu wa viapo unakumbuka?

Heche: Nilisema.

Wakili Katuga: Waambie majaji kama ulitaja vituo ambavyo mawakala walizuiwa.

Heche: Nilisema kwa nchi nzima.

Wakili Katuga: Unajua au hujui kama ukiposhinda uchaguzi, pia ulituhumiwa kufanya fujo na kuingiza kura feki?

Heche: Hilo unajua wewe, sijui.

Wakili Katuga: Unajua au hujui kwamba mwanasiasa akishindwa hakubali kiurahisi?

Heche: CHADEMA ukishindwa unarudi zako nyumbani.

Wakili Katuga: Waambie majaji kama wewe ulivyoshindwa ulikubali?

Heche: Uchaguzi haukuwa huru na haki, nilipoteza.

Wakili Katuga: Ulishinda ubunge mwaka gani?

Heche: 2015.

Wakili Katuga: Uchaguzi wa 2015 ulikuwa huru na haki?

Heche: Uchaguzi wa 2015 ulikuwa na figisu.

Wakili Katuga: Uchaguzi wa 2015 uliochaguliwa uliukubali au uliukataa?

Heche: Niliukubali kwa vita, japo ulikuwa na makosa mengi.

Wakili Katuga: Ulikuwa wa uhuru na haki au haukuwa huru na haki jimboni kwako wewe?

Heche: Haukuwa huru na haki.

Wakili Katuga: Waambie majaji
kama wewe ni mtu wa haki kama unavyojiita, waambie majaji ulikuwa na uwezo wa kuukataa ushindi wako au ulikuwa huna?

Heche: (Heche akawa mbishi, majaji wakamweleza kwamba anaulizwa yeye kwa nafasi yake.)

Wakili Katuga: (Wakili Katuga akarudia swali.)

Heche: Nilikuwa sina uhuru.

 

Kuhusiana na mada hii: