Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, amelishauri Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) lijitenge na Siasa.
Akichangia hotuba ya Wizara ya Ulinzi, leo May 19, 2026, Bungeni Jijini Dodoma, Ado amesema “Jeshi la Wananchi ni Jeshi la ukombozi wa Afrika, ni Jeshi la haki haikuwa kwa bahati mbaya Jeshi hili lilipokelewa Uganda na Kariakoo kwa shangwe, haikuwa kwa bahati mbaya October kwa yale yaliyotokea Jeshi hili lilipokelewa kwa shangwe, natoa changamoto kwa Jeshi, kuna kitu kimoja wakilinde kwa nguvu zote, kitu hicho ndio roho ya thamani yao, Jeshi lijitenge na Siasa, hivi karibuni vimekuwepo vidole… “
Ado hakumalizia mchango wake kwakuwa Spika wa Bunge, Mussa Zungu, amemkatisha akisema “ Mwisho utaaanza kusema vitu nitakuuliza ushahidi utashindwa kaa chini”