"Niwaambie jambo moja kwamba katika uendeshaji wa nchi hakuna majaribio, unampa nchi yule ambaye unamuamini kuwa ataiendesha vyema na maslahi ya wananchi yatapatikana. Na ukiangalia kwetu Tanzania, chama ambacho kweli kitafanya kazi na maslahi ya wananchi yatapatikana ni Chama Cha Mapinduzi peke yake.
"Wengine bado, mkiwapa serikali au jimbo wataenda kuwafuja ama kuwapoteza kwasababu wakiingia kwanza ni kwenda kujifunza lakini utakapompa Jimbo asiyekuwa Chama Cha Mapinduzi anakwenda kuongea na nani? Anaenda kumuomba barabara au maji nani? Kwasababu mwenye serikali ni Chama Cha Mapinduzi yeye ni upinzani.
"Ndugu zangu wa Wilaya hii ya Bunda msicheze na hiyo kitu kabisa. Pelekeni kura kwa wateuliwa wa Chama Cha Mapinduzi. Wapeni kura safari yetu ya maendeleo iendelee," amesema Dk. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa CCM akizungumza na maelfu ya wananchi wa Bunda Mjini leo Oktoba 09, 2025.
Chanzo: Nipashe